CHAMA cha Soka cha Uingereza-FA kimetanagza kuwa timu yao taifa itajipima nguvu kwa ajili ya michuano ya Euro 2016 kwa kucheza mchezo wa kirafiki na Uholanzi katika Uwanja wa Wembley mwakani. Uingereza inayonolewa na Roy Hodgson, ambao walifuzu michuano hiyo bila kufungwa mchezo wowote, watakwaana na Uholanzi ambao wao wameshindwa kufuzu fainali hizo, Machi 29 mwakani. Hiyo itakuwa mara ya 20 kwa timu hizo kukutana huku mara ya mwisho ikiwa Februari mwaka 2012 ambapo Uholanzi ilishinda kwa mabao 3-2. Pamoja na kumaliza katika nafasi ya tatu katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka jana, Uholanzi walishindwa kutamba katika mechi za kufuzu wakimaliza katika nafasi ya nne katika kundi nyuma ya Jamhuri ya Czech, Iceland na Uturuki.
No comments:
Post a Comment