MSHAMBULIAJI wa Tottenham Hotspurs, Harry Kane anategemea wachezaji wa Liverpool kuja na kujituma zaidi wakati watakapokutana Jumamosi hii katika Uwanja wa White Hart Lane kwa mara ya kwanza wakiwa na meneja mpya Jurgen Klopp. Akiwa ametoka katika majukumu ya kimataifa na Uingereza na wachezaji wa Liverpool akiwemo Nathaniel Clyne na Danny Ings, Kane amesema ni jambo ambalo liko wazi kuwa wachezaji wa timu watataka kujionyesha kwa Klopp. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa kutokana na hilo anadhani mchezo huo utakuwa mgumu lakini watajiandaa kwa lolote kuhakikisha wanapata matokeo mazuri. Spurs haijapoteza mchezo toka kuanza kwa msimu na wako katika nafasi ya nane, alama mbili nyuma ya Crystal Palace walioko nafasi ya nne baada ya kuchez michezo nane.
No comments:
Post a Comment