TIMU ya taifa ya Ukraine italazimika kucheza hatua ya mtoano kwa ajili ya kufuzu michuano ya Euro 2016 baada ya kufungwa bao 12-0 nyumbani na mabingwa wa Ulaya Hispania katika mchezo wa mwisho wa kundi D jana. Ukraine ilikuwa ikihitaji matokeo ili kuizidi Slovakia na kufuzu moja kwa moja michuano hiyo lakini ushindi wa nchi hiyo kutoka mashariki mwa Ulaya wa mabao 4-2 dhidi ya Luxembourg uliwahakikishia nafasi ya pili. Hispania wakiwa tayari wamefuzu kama vinara wa kundi hilo, kocha Vicente del Bosque aliwapanga wachezaji wasiokuwa na uzoefu katika mchezo huo uliofanyika huko Kiev. Hispania wamemaliza wakiwa na alama 27, wakifuatiwa na Slovakia wenye alama 22 na Ukraine katika nafasi ya tatu wakiwa na alama 19 huku Belarus, Luxembourg na Macedonia wakiondoshwa.
No comments:
Post a Comment