Tuesday, October 13, 2015

NEYMAR KUSAINI MKATABA MPYA BARCELONA.

MSHAMBULIAJI nyota wa Barcelona, Neymar amesema hana shaka kuwa atakubali kusaini mkataba mpya na mabingwa hao wa La Liga. Wiki iliyopita katibu wa masuala ya ufundi ya klabu hiyo Robert Fernandez alibainisha kuwa mazungumzo ya mkataba mpya na Neymar yalikuwa yakiendelea vyema na kuongeza kuwa ana uhakika nyota huyo atabakia Camp Nou maisha yake yote. Nyota huyo wa kimataifa wa Brazil, amedai mustakabali uko mikononi mwa baba yake ambaye pia ndio wakala wake, lakini akaweka wazi kufurahia maisha katika klabu hiyo. Neymar amesema bado amebakisha miaka mitatu katika mkataba wake na mambo hayo anamuachia baba yake kwani yeye jambo muhimu kwake ni kuisaidia timu ishinde mataji.

No comments:

Post a Comment