Monday, October 5, 2015

ORLANDO PIRATES KUVAANA NA ETOILE DU SAHEL FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO.

KLABU ya Orlando Pitares ya Afrika Kusini imefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho baada ya kufanikiwa kuichapa Al Ahly ya Misri kwa mabao 4-3 katika mchezo wa nusu fainali ya mkondo wa pili iliyofanyika katika Uwanja wa Suez jana usiku. Ushindi huo umeifanya Pirates kutinga fainali kwa jumla ya mabao 5-3 katika mechi mbili walizokutana baada ya kushinda bao 1-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliofanyika huko Soweto. Pirates sasa wataelekea katika fainali ambayo pia itachezwa kwa mikondo miwili dhidi ya Etoile du Sahel ya Tunisia. Nao Etoile walifanikiwa kuwachapa wakongwe wengi wa Misri Zamalek kwa jumla ya mabao 5-4 wakibebwa na ushindi mnono wa mabao 5-1 waliopata katika mchezo wa mkondo wa kwanza kufuatia kupoteza mchezo wao wa marudiano uliochezwa Cairo kwa mabao 3-0 Jumamosi. Fainali ya michuano hiyo inatarajiwa kuchezwa kati ya Novemba 20 au 29 mwaka huu huku Pirates wakianzia nyumbani kabla ya kuifuata Etoile nchini Tunisia.

No comments:

Post a Comment