MGOMBEA urais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa amekanusha vikali kuwa alishiriki kuwatesa wachezaji na kudai ni za uongo. Sheikh Salman anatuhumiwa na kundi la haki za binadamu nchini Bahrain kwa kusaidia kuwatambua wachezaji na wanamichezo wengine waliojihusisha na mandamano ya kutaka demokrasia mwaka 2011. Alikuwa kiongoza wa Chama cha Soka cha Bahrain na mwana familia ya kifalme wakati watu wa usalama walipowakamata watu wengi walioshiriki maandamano hayo. Watu kadhaa walifariki wakati wengine waliokamatwa walifungwa na kuteswa. Akihojiwa Sheikh Salman mwenye umri wa miaka 49 amesema hawezi kukanusha jambo ambalo hajawahi kulifanya na tuhuma kama hizo sio tu zinamharibia hadhi yake lakini pia zinaumiza.
No comments:
Post a Comment