MENEJA wa Manchester United, Louis van Gaal amepuuza ukosolewaji uliotolewa na kiungo wa zamani Paul Scholes kuhusu jinsi timu inavyocheza, akidai kuwa fimbo na mawe vinaweza kumvunja mfupa lakini majina hayamuumizi. Kiungo huyo wa zamani ambaye ameichezea United mechi 718, amesema asingefurahia kucheza akiwa chini ya Van Gaal kwani kikosi hicho kimekuwa na mapungufu katika masuala ya ubunifu. Kauli ya Scholes imekuja kufuatia United kung’olewa katika michuano ya Kombe la Ligi jana. Van Gaal aliwaambiwa wanahabari kuwa Scholes alikuwa hana wajibu wa kutoa kauli kwani hafahamu ilikuwa na manufaa kwa nani.
No comments:
Post a Comment