Thursday, November 26, 2015

BLATTER AIVIMBIA KAMATI YA MAADILI.

RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Sepp Blatter aliyesimamishwa amedai kuwa anaamini Mkutano Mkuu wa shirikisho hilo pekee ndio wenye uwezo wa kumuondoa madarakani na sio kamati ya maadili. Akijifananisha na rais wa nchi, Blatter amesema hakuna mtu wa kawaida anayeweza kumfukuza rais aliyechaguliwa zaidi ya bunge pekee. Rais huyo aliendelea kudai kuwa yeye sio ofisa wa wa FIFA bali ni rais aliyechaguliwa katika Mkutano Mkuu na kama kuna mtu habaliani na anavyofanya shughuli zake anapaswa kuwageukia wajumbe wa mkutano huo waliomchagua. Blatter amesema rais wa FIFA huwa anachaguliwa na wajumbe kutoka mashirikisho 209 na kila mmoja wao anapiga kura moja hivyo ni aibu kwake kwa kamati ya maadili kuja maamuzi ya kumsimamisha asiingie ofisini. Blatter alisimamishwa kwa siku 90 sambamba na makamu wake Michel Platini kwa tuhuma ya kufanya malipo yaliyoaminika ya paundi milioni 1.35 kwenda kwa rais huyo wa Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA mwaka 2011, ingawa wote wawili wamekanusha kufanya lolote baya.

No comments:

Post a Comment