Thursday, November 26, 2015

ISCO AFUNGIWA MECHI MBILI.

KIUNGO wa Real Madrid, Isco amepewa adhabu ya kufungiwa michezo miwili jana kwa kosa la kumkwatua nyota wa Barcelona Neymar katika mchezo baina ya timu uliochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita. Katika mchezo huo wa La Liga maarufu kama Clasico uliofanyika katika Uwanja wa Santiago Barnabeu, Madrid alibugizwa mabao 4-0. Nyota huyo wa kimataifa wa Hispania, alikuwa ndio kwanza ameingia akitokea benchi katika kipindi cha pili kabla ya kufanya tukio hilo. Adhabu hiyo itamfanya Isco kukosa mechi ya ugenini ambapo Madrid wataifuata Eibar Jumapili hii pamoja na ule dhidi ya Getafe utakaofanyika Desemba 5 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment