Wednesday, November 25, 2015

MULLER AWAPIGA BAO MESSI NA RONALDO.

MSHAMBULIAJI wa Bayern Munich, Thomas Muller amekuwa mchezaji mdogo zaidi kupata ushindi wa mechi 50 za Ligi ya Mabingwa Ulaya kufuatia timu hiyo kuichapa Olympiakos jana. Muller akiwa na umri wa miaka 26 amefikia rekodi hiyo akiwa mdogo kwa mwaka mmoja kuliko Lionel Messi na karibu mdogo kwa miaka miwili kuliko Cristiano Ronaldo. Nyota huyo wa kimataifa wa Ujerumani ambaye alicheza michuano hiyo kwa mara ya kwanza Macho mwaka 2009, alifunga bao moja katika ushindi wa mabao 4-0 waliopata dhidi ya Olympiakos. Akihojiwa Muller ambaye amefikia rekodi kwa kucheza mechi 75, amesema amefikia rekodi hiyo kwasababu anacheza katika klabu nzuri. Naye nahodha wa Bayern Philipp Lahm alimtania Muller kwa kumwambi kuwa anapaswa kuwanunulia vinywaji kwasababu wamekuwa sehemu kubwa ya mafanikio hayo.

No comments:

Post a Comment