Wednesday, November 25, 2015

ERIKSSON AMTAKA ROONEY KUFIKIRIA KWENDA CHINA.

KOCHA wa zamani wa Uingereza, Sven-Goran Eriksson amesema Wayne Rooney ataipaisha Ligi Kuu ya China na kumtaka mshambuliaji huyo wa Manchester United kufikiria kuhamia huko kama akija kuondoka Old Trafford. Eriksson ambaye kwasasa anainoa klabu ya Shanghai SIPG, amesema mchezo wa soka umekuwa ukiwa kwa kiwango cha kawaida nchini humo lakini ujio wa Rooney unaweza kusaidia kulikuza zaidi soka la huko. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa soka limekuwa kitu kikubwa nchini humo na uwepo wa nyota kama Robinho, Asamoah Gyan na Demba Ba umeleta vitu tofauti katika ligi. Eriksson amesema kutokana na uwezo wa juu alionao Rooney unaweza kulipeleka soka la huko katika viwango vingine.

No comments:

Post a Comment