Wednesday, November 25, 2015

GERRARD KUANZA MAZOEZI LIVERPOOL WIKI IJAYO.

NGULI wa zamani wa Liverpool, Steven Gerrard amethibitisha kurejea katika klabu hiyo wiki ijayo lakini kwa ajili ya kufanya mazoezi pekee. Kiungo huyo mkongwe wa klabu ya Los Angeles Galaxy mwenye umri wa miaka 35 amekuwa akihusishwa na tetesi za kurejea kufuatia msimu wa Ligi Kuu ya Marekani-MLS kusimama. Lakini nyota huyo wa zamani wa Uingereza alikanusha tetesi hizo na kudai kuwa atakwenda Anfield kwa ajili ya kufanya mazoezi chini ya meneja wa sasa Jurgen Klopp. Akihojiwa Gerrard amesema ana hamu kubwa ya kujifunza kutoka kwa Mjerumani huyo wakati atapokwenda kufanya nao mazoezi wiki ijayo. Gerrard ameitumikia Liverpool kwa miaka 17 kabla ya kuamua kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu uliopita.

No comments:

Post a Comment