Wednesday, November 25, 2015

DORTMUND KUMPIGANIA AUBAMEYANG.

KLABU ya Borussia Dortmund imedai itapambana kufa na kupona kuhakikisha wanabaki na mshambuliaji wao nyota Pierre Emerick Aubameyang. Vilabu kadhaa vikubwa barani Ulaya tayari vimeanza kummezea mate nyota huyo wa kimataifa wa Gabon kutokana na kiwango kikubwa katika ufungaji walichokionyesha msimu huu. Ofisa mkuu wa Dortmund Hans-Joachim Watzke amesema watapambana kadri wawezavyo kuhakikisha wanabaki na nyota huyo ambaye mpaka ameshafunga mabao 22. Watzke aliendelea kudai kuwa wachezaji wengine watakaopambana ili kuwabakisha ni pamoja na Matis Hummels, Ilkay Gundogan, Marko Reus na Henrikh Mkhitaryan.

No comments:

Post a Comment