Wednesday, November 25, 2015

KIPA WA ROMA AIFAGILIA BARCELONA.


GOLIKIPA wa AS Roma, Wojciech Szczesny amekiri kuwa kikosi chao kilikuwa kikicheza dhidi ya timu kutoka sayari nyingine baada ya Barcelona kuwararua kwa mabao 6-1 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya uliochezwa jana. Szczesny alikosa nguvu ya kuwazuia Barcelona waliokuwa katika kiwango chao cha juu katika mchezo huo uliochezwa Camp Nou, huku nyota wake Lionel Messi na Luis Suarez wakifunga mabao mawili kila mmoja. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Szczesny amesema uliokuwa mzuri kuutizama kwasababu walikuwa wakicheza dhidi ya timu kutoka sayari nyingine. Kipa huyo aliendelea kudai kuwa alikuwa langoni akiichezea Roma lakini anafurahia alichokiona kwa timu pinzani kwani walikuwa wakicheza vyema na ilikuwa raha kuwatizama hata kama wamefungwa.

No comments:

Post a Comment