Wednesday, November 25, 2015

MOURINHO ALAUMU NYASI ZA UWANJA KUFUATIA TERRY KUUMIA.

MENEJA wa Chelsea, Jose Mourinho amelaumu nyasi za uwanja kusababisha majeruhi ya kifundo cha mguu ambayo yanaweza kumzuia nahodha John Terry kutocheza katika mchezo wa Ligi Kuu Jumapili hii dhidi ya Tottenham Hotspurs. Terry mwenye umri wa miaka 34 alitolewa nje katika machela katika dakika ya 72 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Maccabi Tel Aviv ambao walishinda mabao 4-0. Akihojiwa Mourinho amesema anafahamu kikubwa kilichosababisha Terry kuumia katika mchezo huo ni hali mbaya ya uwanja. Mapema kabla ya mchezo huo kocha huyo alilaumu uwanja huo wa Sammy Ofer kuwa na nyasi mbaya kufuatia kiungo wake Ramires kuumia wakati wa mazoezi Jumatatu.

No comments:

Post a Comment