Thursday, November 26, 2015

PELLEGRINI AMLILIA JOE HART.

MENEJA wa Manchester City, Manuel Pellegrini amesema ni ngumu kujua muda atakaokaa nje Joe Hart baada ya kupata majeruhi jana katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya ambao walifungwa na Juventus. Hart mwenye umri wa miaka 28 alibadilishana na golikipa wa kimataifa wa Argentina Wiily Caballero mwneye umri wa miaka 34 katika dakika za majeruhi kwenye mchezo huo waliofungwa bao 1-0. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo, Pellegrini amesema Hart alipata majeruhi ya msuli hivyo ni ngumu kujua ni muda gani haswa atakaa nje kwa wakati huu lakini kama watamkosa ana imani na Caballero kuziba nafasi yake. Bao pekee katika mchezo huo liliwekwa kimiani na nyota wa Juventus Mario Mandzukic ingwa hata hivyo wote wamefuzu hatua inayofuata katika kundi D.

No comments:

Post a Comment