Thursday, November 26, 2015

FLAMINI ATAMBA KUZIBA VYEMA NAFASI ZA COQUELIN NA ARTETA.

KIUNGO Mathieu Flamini ana uhakika anaweza kuisaidia Arsenal kuziba pengo la majeruhi Francis Coquelin na Mikel Arteta na adhabu muda mwingine wa kucheza utamsaidia kupandisha kiwango chake. Coquelin amesema wakicheza vyema katika safu ya kiungo wa ulinzi lakini anatarajiwa kukaa nje kwa miezi mitatu baada ya kupata majeruhi katika mchezo wa Jumamosi iliyopita dhidi ya West Bromwich Albion huku Arteta naye akitarajiwa kukaa nje mwezi mmoja baada ya kupata majeruhi katika mchezo huohuo. Flamini ambaye yuko katika msimu wa mwisho katika mkataba wake amepania kuitumia vyema nafasi nafasi hiyo. Akihojiwa Flamini amesema muda mwingine sababu zinaweza kuwa nyingi hivyo inabidi ukubali kukaa benchi lakini ukipata nafasi unapaswa kuonyesha kuwa bado unaweza kucheza katika kikosi cha Arsenal. Arsenal itakabiliwa na kibarua kizito dhidi ya Norwich City katika mchezo wa Ligi Kuu utakaochezwa Jumapili hii.

No comments:

Post a Comment