CHAMA cha Soka cha Uingereza, kimemfungia mechi moja na kumtoza faini ya paundi 40,000 meneja wa Chelsea Jose Mourinho. Adhabu hiyo imekuja baada ya Mourinho kukiri kosa kwa kutumia lugha chafu wakati kikosi chake kilipofungwa na West Ham United Octoba 24 mwaka huu. Mourinho mwenye umri wa miaka 52 aliondolewa katika benchi lake la ufundi uwanjani na kuamriwa kwenda jukwaani baada ya kwenda kuzungumza na mwamuzi Jon Moss katika chumba chake wakati wa mapumziko. Meneja huyo sasa anatarajiwa kuukosa mchezo wa Ligi Kuu ambao Chelsea itakwaana na Stoke City Jumamosi hii.
No comments:
Post a Comment