NAHODHA wa zamani wa kimataifa wa Uingereza, Steven Gerrard amebainisha kuwa anafikiria kustaafu soka rasmi mwishoni mwa msimu wa 2016 kufuatia klabu ya Los Angeles Galaxy kuenguliwa katika mtoano. Mkongwe huyo wa zamani wa Liverpool, mwenye umri wa miaka 35 alijiunga na Galaxy Julai mwaka huu kwa mkataba wa miezi 18, akifunga mabao mawili na kusaidia mengine matatu katika mechi 14 za Ligi alizocheza katika msimu wake wa kwanza. Galaxy walienguliwa katika michuano ya Kombe la MLS na Seatrle Sounders kwa kipigo cha mabao 3-2 na Gerrard ameamua kutundika daruga zake rasmi mwakani baada ya kulikosa taji hilo. Akihojiwa Gerrard amesema msimu ujao unaweza kuwa wa mwisho kwake kama mchezaji kwani anapenda kumaliza soka akiwa bado yuko katika kiwango cha juu.
No comments:
Post a Comment