KIUNGO wa Chelsea, Cesc Fabregas amekanusha tuhuma za vyombo vya habari kuwa ndiye kinara wa kutengeneza mgomo katika vyumba vya kubadilisha nguo kumpinga meneja wao Jose Mourinho. Blog moja ya michezo nchini Uingereza imedai Fabregas ndio alikuwa kinara wa mgomo baridi katika klabu hiyo ambayo ndio mabingwa watetezi wa Ligi Kuu. Akitumia ukurasa wa mtandao wa kijamii wa twitter, Fabregas alikanusha taarifa hizo zilizozagaa dhidi yake akidai kuwa anafurahia maisha katika klabu hiyo na amekuwa na mahusiano mazuri na Mourinho. Kiungo huyo aliendelea kudai kuwa kuna watu wachache kutoka nje wanataka kuiyumbisha klabu lakini anaamini wanaweza kuyapita magumu hayo na kuimarika kama zamani. Chelsea ambao wamepoteza michezo yao sita kati ya 11 waliyocheza msimu huu wanashikilia nafasi ya 15 katika msimamo wa ligi.
No comments:
Post a Comment