Tuesday, November 3, 2015

SAMATTA AZIDI KUNG'AA AFRIKA.

NYOTA ya mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta imeendelea kung’aa kufuatia kuingia katika orodha ya wachezaji 10 bora watakaogombania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Afrika kwa wachezaji wa ndani. Shirikisho la Soka la Afrika-CAF lilipunguza orodha hiyo kutoka wachezaji wachezaji 23 iliyowatangaza hapo awali mpaka kubakia wachezaji 10 ambao nao watachunjwa na kubakia watatu. Mwaka unaonekana kuwa mzuri kwa Samatta kwani mbali na kuingia katika orodha hiyo lakini pia timu yake ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC iko katika hatua ya fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa ya Afrika. Samatta amekuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Mazembe akifunga mabao yaliyoiwezesha kutinga hatua hiyo huku pia akifunga bao katika mchezo wa fainali ya mkondo wa kwanza iliyochezwa Jumamosi iliyopita huko Algeria na kuifanya timu hiyo kuongoza kwa mabao 2-1 dhidi ya USM Algier. Tuzo hiyo itatolewa katika hafla maalumu itakayofanyika Januari 7 mwakani jijini Abuja, Nigeria.

Orodha kamili ya wachezaji hao nchi na klabu wanazotoka ni pamoja na:
Abdeladim Khadrouf (Morocco & Moghreb Tetouan)
Baghdad Bounedjah ( Algeria & Etoile du Sahel)
Felipe Ovono (Equatorial Guinea & Orlando Pirates)
Kermit Erasmus (South Africa & Orlando Pirates)
Mohamed Meftah ( Algeria & USM Alger)
Mudather Eltaib Ibrahim ‘Karika’ (Sudan & El Hilal)
Robert Kidiaba Muteba ( DR Congo & TP Mazembe)
Roger AssalĂ© (Cote d’Ivoire & TP Mazembe)
Zineddine Ferhat (Algeria & USM Alger)

No comments:

Post a Comment