Tuesday, November 3, 2015

TUZO YA TANO YA MCHEZAJI BORA WA AFRIKA YANUKIA KWA TOURE.

KIUNGO wa kimataifa wa Ivory Coast Yaya Toure ni miongoni mwa wachezaji 10 walioteuliwa katika orodha ya kushindania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Afrika, ikiwa ni mara yake ya tano mfululizo. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 32 anayechezea Manchester City ya Uingereza alishinda tuzo hiyo mara ya kwanza 2011 na akishinda mwaka huu itakuwa mara yake ya tano. Akifanikiwa kutwaa tuzo hiyo, atakuwa amempita Samuel Eto'o ambaye ameshinda tuzo hiyo mara nne. Mshindi ataamuliwa kwa wingi wa kura zitakazopigwa na makocha au wakurugenzi wa kiufundi wa mataifa wanachama wa CAF. Tuzo hiyo itatolewa kwenye hafla itakayoandaliwa Alhamisi, Januari 7, 2016 mjini Abuja, Nigeria.

Orodha kamili ndiyo hii:Andre Ayew (Ghana & Swansea)
Aymen Abdennour (Tunisia & Valencia)
Mudather Eltaib Ibrahim 'Karika' (Sudan & El Hilal)
Mohamed Salah (Egypt & Roma)
Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon & Borussia Dortmund)
Sadio Mane (Senegal & Southampton)
Serge Aurier (Cote d'Ivoire & Paris Saint Germain)
Sofiane Feghouli (Algeria & Valencia)
Yacine Brahimi ( Algeria & Porto)
Yaya Toure (Cote d'Ivoire & Manchester City)

No comments:

Post a Comment