GOLIKIPA wa zamani wa Sunderland na Ipswich Town, Marton Fulop amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 32. Nyota huyo wa zamani wa kimataifa wa Hungary, alifanyiwa upasuaji kuondoa uvimbe wa saratani mkononi mwaka 2013 lakini aliruhusiwa kuendelea kucheza soka. Fulop ameiwahi kuichezea Sunderland mechi 47 kati ya mwaka 2006 mpaka 2010 kabla ya kuibukia Ipswich mwaka 2011. Golikipa huyo pia amewahi kucheza katika klabu za Tottenham Hotspurs na West Bromwich Albion pamoja na kuchukuliwa kwa mkopo katika klabu za Chesterfield, Coventry, Leicester City, Stoke City na Manchester City.
No comments:
Post a Comment