MWENYEKITI wa Chama cha Soka cha Uingereza-FA ametania kuwa watapaswa kujiua wenyewe kama timu ya taifa ya nchi hiyo itashindwa kuvuka hatua ya makundi katika michuano ya Euro 2016. Uingereza inayonolewa na Roy Hodgson imepangwa sambamba na timu za Wales, Urusi na Slovakia katika michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Juni 10 huko Ufaransa. Akihojiwa Dyke amesema ni lazima wavuke kundi hilo na kama wakishindwa hiyo itakuwa ni habari mbaya kwa soka la Uingereza. Dyke aliongeza kuwa anaamini Uingereza inaweza kushinda taji la Kombe la Dunia katika miaka ya karibuni.
No comments:
Post a Comment