KAMATI ya maadili ya Shirikisho la Soka Duniani-FIFA imemuongeza adhabu katibu mkuu Jerome Valcke kwa kumsimamisha kwa zingine 45 kujishughulisha na masuala yeyote ya soka. Adhabu ya kusimamishwa kwa siku 90 aliyopewa Valcke ilikuwa imemalizika jana lakini mwenyekiti wa kamati hiyo Cornel Borbely alitaka kuongezwa kwa siku nyingine zaidi jambo ambalo lilipitishwa. Katika taarifa ya kama hiyo, imedai kufikia uamuzi huo kutokana na kutokamilika kwa uchunguzi na adhabu hiyo itaanza rasmi leo. Valcke amekuwa akihusishwa na sakata la kuuza tiketi za Kombe la Dunia lililofanyika nchini Brazil mwaka 2014 kwa bei isiyo halali. Kamati hiyo inapendekeza Valcke afungiwe miaka tisa kutojihusisha na masuala ya michezo kutokana na tuhuma hizo za ufisadi.
No comments:
Post a Comment