MENEJA wa Liverpool, Jurgen Klopp amekiri anaweza kulazimika kusajili baada ya matatizo ya majeruhi kuzidi katika kikosi chake wakati walipopata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Stoke City kwenye mchezo wa nusu fainali ya mkondo wa kwanza ya Kombe la Ligi jana. Nyota wake Philippe Coutinho na Dijan Lovren walitolewa nje kutokana na amjeruhi ya msuli ya paja na Kolo Toure naye alimaliza mchezo huo akionekana kuwa na tatizo kama hilo. Mara kadhaa Klopp amekuwa akidai kuwa hatanunua mchezaji mpya katika kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo. Lakini kutokana na majeruhi kuzidi kuongezeka, Klopp amesema anadhani anaweza kulazimika kuongeza nguvu katika kikosi chake. Kuumia kwa Toure na Lovren kunaifanya Liverpool kukosa beki wa kati aliye fiti kwani Martin Skrtel na Mamadou Sakho nao pia ni majeruhi.
No comments:
Post a Comment