Monday, January 11, 2016

MONREAL KUONGEZA MKATABA ARSENAL.

MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amethibitisha kuwa Nacho Monreal anakaribia kukubalia kusaini mkataba mpya. Taarifa zinadai kuwa, beki huyo wa kushoto ambaye mkataba wake wa sasa unamalizika mwaka 2017, anatarajiwa kusaini mkataba mpya ambao utamuweka Emirates mpaka mwaka 2019. Akihojiwa Wenger amesema wako katika mazungumzo ya mwishoni kuhusu mkataba mpya wa Monreal na pindi ukikamilika watatangaza. Monreal alijiunga na Arsenal akitokea Malaga Januari mwaka 2013 na amekuwa akihusishwa na tetesi za kuhamia Athletic Bilbao kiangazi mwaka jana.

No comments:

Post a Comment