KLABU ya Bayern Munich inatarajiwa kuingia katika mbio za kumuwania mshambuliaji wa Bayer Leverkusen Javier Hernandez majira ya kiangazi. Hernandez amekuwa akionyesha kiwango bora toka ajiunge na Leverkusen kiangazi mwaka jana ambapo amefunga mabao 21 mpaka sasa. Carlo Ancelotti ambaye atachukua mikoba ya Pep Guardiola majira ya kiangazi, aliwahi kumnoa mchezaji huyo wakati alipokwenda kwa mkopo Real Madrid akitokea Manchester United na taarifa zinadai kuwa maofisa wa Bayern wanapigana ili kumsajili nyota huyo wa kimataifa wa Mexico. Hernandez pia amesema alikuwa akifurahia kufanya kazi na Ancelotti ambaye alimpa nafasi akiwa Madrid.
No comments:
Post a Comment