Monday, February 8, 2016

TERRY ADAI HAKUNA LOLOTE JIPYA KATI YAKE NA CHELSEA.

NAHODHA wa Chelsea, John Terry amesema kumekuwa hakuna mawasiliano yeyote kati yake na klabu pamoja na meneja wake Guus Hiddink kusisitiza kuwa anaweza kubakia. Terry mwenye umri wa miaka 35, alidai wiki iliyopita kuwa hajapewa ofa yeyote ya mkataba mpya wakati huu wake wa sasa ukielekea kumalizika mwishoni mwa msimu huu. Akiulizwa baada ya mchezo wa jana ambao walitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Manchester United kama kuna lolote lililobadilika Terry alidai hakuna lolote lililobadilika. Terry amesema alishaweka wazi nia yake ya kubakia lakini hakuna mawasiliano yeyote yaliyofanywa kati yake na klabu mpaka sasa.

No comments:

Post a Comment