Friday, February 5, 2016

ROSICKY PANCHA TENA.

KIUNGO wa Arsenal, Tomas Rosicky anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi mitatu kwasababu ya majeruhi ya msuli. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 35, ambaye mkataba wake unamalizika majira ya kiangazi mwaka huu, alipata majeruhi hayo katika mchezo dhidi ya Burnely Jumamosi iliyopita. Nyota huyo wa kimataifa wa Jamhuri ya Czech, alijiunga na Arsenal Mei mwaka 2006. Kwa upande mwingine meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amethibitisha mshambuliaji Danny Welbeck atarejea tena uwanjani katika mchezo wa vijana chini ya umri wa miaka 21 leo. Welbeck alikuwa nje ya uwanja toka April mwaka jana baada ya kuumia katika mchezo dhidi ya Chelsea uliomalizika kwa sare ya bila kufungana.


No comments:

Post a Comment