NAHODHA wa zamani wa Italia, Fabio Cannavaro ametimuliwa kuifundisha klabu ya Al-Nassr ya Saudi Arabia. Cannavaro alipewa michezo 22 kuisaidia Al-Nassr kutetea taji lao la Ligi Kuu maarufu kama Saudi Pro League, lakini utaratibu huo ulikatishwa akiwa ameitukia klabu hiyo kwa mechi 12 kufuatia kipigo cha mabao 4-3 walichopata kutoka kwa Narjan jana. Beki huyo wa zamani wa Juventus ambaye aliondoka katika klabu ya Guangzhou Evergrande Taobao Juni mwaka jana, alipewa mikoba ya kuinoa timu hiyo Octoba mwaka jana kufuatia kuondoka kwa Jorge da Silva. Sababu kubwa ya kutimuliwa kwake na kushindwa kuisaidia timu hiyo kupambania kutetea taji lao la ligi. Al-Nassr inashika nafasi ya sita katika msimamo wa ligi, wakiwa alama 18 nyuma ya vinara Al Hilal huku wakiwa wameshinda mechi moja pekee toka kuanza kwa mwaka huu.
No comments:
Post a Comment