KIUNGO wa Chelsea, Oscar amesema kuwa hana sababu ya kuodoka katika klabu hiyo na amepanga kuwaongezea mataji zaidi mabingwa hao wa Ligi Kuu. Nyota huyo wa kimataifa wa Brazil, amesema anataka kuendelea kubakia Chelsea kwa kipindi kirefu ili kulipa fadhila kwa upendo alioonyeshwa na mashabiki wa klabu hiyo. Oscra ambaye mkataba wake wa sasa unamalizika mwaka 2019, aliendelea kudai kuwa hana sababu yeyote ya kuondoka kwa kila mtu anammpenda na pia anafurahia kuwepo hapo. Chelsea ambao kwasasa wanashika nafasi ya 13 katika msimamo wa Ligi Kuu, wanatarajiwa kupambana na Newcastle United kesho.
No comments:
Post a Comment