KIUNGO wa Shakhtar Donetsk Alex Teixeira anakaribia kusajiliwa kwa kitita cha euro milioni 50 kwenda nchini China. Taarifa za mwanzoni zilidai kuwa Liverpool walikuwa katika mzungumzo na Shakhtar kwa ajili ya kumuwania nyota huyo wakati dirisha dogo la usajili lilipokuwa wazi lakini walishindwa baada ya thamani ya mchezaji huyo kupandishwa kutoka paundi milioni 38 mpaka kufikia paundi milioni 53 ndani ya muda wa siku tatu. Liverpool walikuwa wakitarajiwa kujaribu tena uwezekano wa kumnasa majira ya kiangazi lakini taarifa zilizozagaa nchini Italia sasa zinadai kuwa mazungumzo kati ya Shakhtar na Jiangsun Suning yanaendelea huku dili likitegemewa kukamilika. Jiangsun Suning tayari wameshamsajili kiungo Ramires kutoka Chelsea kwa ada inayoaminika kufikia paundi milioni 25.
No comments:
Post a Comment