Wednesday, February 3, 2016

KESI ZAZIDI KUMUANDAMA NEYMAR.

WAENDESHA mashtaka nchini Brazil wamependekeza kwamba nyota wa Barcelona Neymar ashtakiwe na mashtaka matatu ya ufisadi kuhusu kesi ya kodi wakati wa uhamisho wake kwenda Barcelona. Inadaiwa kwamba kampuni zilibuniwa kutumika kwa niaba yake ili mchezaji huyo alipe kodi ya kiwango cha chini. Maafisa nchini Brazil wamesema kuwa madai hayo dhidi ya mshambuliaji huyo yanasimamia kipindi cha miaka saba kuanzia 2006. Madai hayo ni tofauti na yale ya kesi yake iliyosikizwa siku ya jana nchini Uhispania. Neymar alihudhuria kesi yake ya madai ya ufisadi kuhusu uhamisho wake kutoka Santos kwenda Barcelona ambapo amekana kufanya makosa yoyote. Waendesha mashtaka wa serikali ambao wanapendekeza kushtakiwa kwake wanadai kwamba kampuni zilibuniwa na fedha ambazo zingelipishwa kodi katika kiwango cha mtu binafsi zilitumwa katika kampuni hizo ili kupunguza ada hiyo.

No comments:

Post a Comment