KLABU ZA CHINA ZENDELEZA KUFURU, BAADA YA MOJAWAPO KUMNASA NYOTA WA ATLETICO KWA KITITA CHA PAUNDI MILIONI 31.
KLABU ya Guangzhou Evergrande inayoshiriki Ligi Kuu ya China maarufu kama Super League imevunja rekodi ya usajili ya nchi hiyo kwa kumsajili nyota wa Atletico Madrid Jackson Martinez kwa kitita cha paundi milioni 31. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Colombia amesaini mkataba wa miaka minne na anataraji kujiunga na mazoezi ya kipindi cha baridi Februari 9 huko Dubai baada ya kufanyiwa vipimo vya afya. Nyota huyo amefunga mabao matatu katika mechi 22 alizoichezea Atletico toka anunuliwe kwa kitita cha paundi milioni 24.8 kutoka FC Porto kiangazi mwaka jana. Martinez ni mchezaji mwingine mwenye jina kubwa kusajili nchini China mwaka huu baada ya kiungo wa Chelsea Ramires na Gervinho aliyetokea AS Roma. Meneja wa Martinez katika klabu hiyo atakuwa kocha wa zamani wa Chelsea na Brazil Luiz Felipe Scolari, wakati kiungo wa zamani wa Tottenham Hotspurs Paulinho na Robinho watakuwa wachezaji wenzake katika timu hiyo.
No comments:
Post a Comment