Tuesday, February 2, 2016

NEYMAR KUIBUKIA MAHAKAMANI.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Brazil na klabu ya Barcelona, Neymar anatarajiwa kutoa ushahidi katika mahakama moja nchini Hispania kuhusu madai ya ufisadi yanayozunguka uhamisho wake. Aliyekuwa rais wa Barcelona Sandro Rossel na rais wa sasa Josep Maria Bartomeu wamekana kufanya makosa yeyote katika uhamisho wa nyota huyo jana. Barcelona ilidai kulipa kiasi cha euro milioni 57 katika usajili wa Neymar mwaka 2013 huku wazazi wake nao wakipokea euro milioni 40 na klabu ya Santos aliyotokea wakichukua euro milioni 17. Uchunguzi umebaini kuwa ada ya nyota huyo ilifikia karibu euro milioni 83 na Barcelona wakituhumiwa kuficha kiasi kikubwa cha mkataba huo. Kesi hiyo iliwasilishwa mahakamani na kampuni ya uwekezaji ya DIS ambayo ilimiliki asilimia 40 ya haki za nyota huyo wakidai kupunjwa haki yao kwa kuambulia euro milioni 6.8 kati ya euro milioni 17 walizopewa Santos.

No comments:

Post a Comment