MABINGWA watetezi Chile, wamepangwa katika kundi moja la D sambamba na Argentina, Bolivia na Panama katika michuano ya Copa Amerika 2016. Chile waliitandika Argentina kwa changamoto ya mikwaju ya penati mwaka jana na kushinda taji lao la kwanza kubwa katika historia. Michuno mikongwe kabisa ya kimataifa ambayo inatimiza miaka 100, itashuhudia wenyeji Marekani wakipambana na Colombia, Costa Rica na Paraguay wakivaana katika kundi A. Uruguay ambayo ndio timu iliyopata mafanikio zaidi katika michuano hiyo wenyewe wamepangwa na Jamaica, Mexico na Venezuela katika kundi C wakati mabingwa wa mwaka 2007 Brazil wao watakuwa na Ecuador, Haiti na Peru katika kundi B. Michuano hiyo ya mwaka huu imeongeza timu nne na imekuwa ya kwanza kufanyika nje ya Shirikisho la Soka la Amerika Kusini-COMNEBOL. Michuano hiyo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Juni 3 kwa marekani kufungua dimba na Colombia huko Santi Clara, California huku fainali ikitarajiwa kuchezwa June 26 katika Uwanja wa MetLife uliopo East Rutherford, New Jersey.
No comments:
Post a Comment