Sunday, March 27, 2016

KOCHA WA UINGEREZA AWAPONGEZA WACHEZAJI WAKE KWA KUICHAPA UJERUMANI.



KOCHA wa timu ya taifa ya Uingereza, Roy Hodgson amesema kutoka nyuma kwa kikosi chake na kuja kushinda mchezo dhidi ya mabingwa wa dunia Ujerumani jana, ilikuwa moja kati ya siku nzuri akiwa kama meneja wa timu hiyo. Bao la dakika za majeruhi lililofungwa na Eric Dier liliwahakikishia ushindi wa mabao 3-2, baada ya Uingereza kutoka nyuma kufuatia kufungwa mabao mawili katika mchezo huo uliofanyika katika Uwanja wa Olimpiki jijini Berlin. Akihojiwa Hodgson amesema pamoja na kwamba ulikuwa mchezo wa kirafiki lakini kikosi chake kilicheza vyema ingawa bado wana safari ndefu ili waweze kuwafikia mabingwa hao wa dunia. Toni Kroos na Mario Gomez ndio waliofunga mabao ya Ujerumani kabla ya Harry Kane na Jamie Vardy aliyeingia akitokea benchi hawajasawazisha. Hodgson alichukua mikoba ya kuinoa Uingereza kutoka kwa kocha aliyejizulu nafasi hiyo Fabio Capello kuelekea katika michuano ya Euro 2012 ambako walitolewa katika hatua ya robo fainali na Italia.

No comments:

Post a Comment