KIUNGO mahiri wa Arsenal, Mesut Ozil anadaiwa kuwa anaweza kuondoka majira ya kiangazi kama Arsene Wenger ataendelea kuinoa klabu hiyo msimu ujao. Nyota huyo wa kimataifa wa Ujerumani amekuwa katika kiwango bora msimu huu lakini amechoshwa na ukame wa mataji na hataki kuendelea kuichezea timu hiyo chini ya Wenger. Taarifa hizo zinaendelea kudai kuwa Ozil na wakala wake tayari wameanza kuangalia uwezekano wa kurejea La Liga ingawa rais wa Real Madrid Florentino Perez hana shauku sana ya kumrejesha kiungo huyo Santiago Bernabeu. Hatua hiyo inaweza kuwaruhusu Atletico Madrid kupata nafasi kama wakiweza kulipa mshahara wa kiungo huo wakati Valencia na Sevilla nazo zikidaiwa kumuwania.
No comments:
Post a Comment