Tuesday, April 5, 2016

BARCELONA YAZIKEMEA KLABU ZINAZOMMEZEA MATE NEYMAR.

RAIS wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu amesisitiza klabu hiyo haina mpango wowote wa kumuuza Neymar na hataruhusu klabu yeyote kuanza mazungumzo na nyota huyo wa kimataifa wa Brazil. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 amekuwa akihusishwa na tetesi za kuwania na mahasimu wao Real Madrid na mabingwa Legue 1 Paris Saint-Germain katika miezi ya karibuni wakati mazungumzo ya mkataba mpya yakiwa bado yanaendelea. Barcelona wana uhakika kuwa Neymar ambaye mkataba wake wa sasa unamalizika 2018 atasaini mkataba mpya lakini wakala wake alidokeza mapema wiki hii kuwa nyota huyo wa zamani wa Santos anaweza kuvutiwa na uhamisho wa kwenda PSG. Bartomeu ana uhakika Barcelona hawataweza kumuuza nyota huyo, ingawa klabu yeyote itakayomuhitaji italazimika kulipa kitita cha euro milioni 193 ili kuvunja mkataba wake wa sasa. Neymar amekuwa katika kiwango bora msimu huu akiwa amefunga mabao 27 katika mechi 39 za mashindano yote alizoichezea Barcelona.

No comments:

Post a Comment