Tuesday, April 5, 2016

UNITED KUMPA VAN GAAL EURO MILIONI 100 ZA USAJILI KIANGAZI.

KLABU ya Manchester United iadaiwa kujipanga kumpa Louis van Gaal kitita cha euro milioni 100 kwa ajili ya usajili wa kujiandaa na msimu ujao huku Romelu Lukaku akidaiwa kuwepo katika orodha ya juu ya wachezaji wanaomtaka. United imeshafanya usajili kadhaa wa fedha nyingi toka Mholanzi huyo alipoteuliwa mwaka 2014 lakini bado hajaonyesha matokeo mazuri hivyo kumuacha katika shinikizo huku mwenye akikiri anaweza kutimuliwa kiangazi. Hata hivyo United wanaweza kuamua kubaki na meneja huyo wa zamani wa Barcelona na kumkabidhi kitita kikubwa kwa ajili ya kuimarisha kikosi chake majira ya kiangazi. Mshambuliaji wa Everton Lukaku amekuwa akizivutia klabu nyingine kutokana na kuwa msimu mzuri akifunga mabao 18 katika mechi 30 za Ligi Kuu na United wameripotiwa kuwa tayari kutoa ofa kwa ajili yake majira ya kiangazi.

No comments:

Post a Comment