KIUNGO wa Wolfsburg, Andre Schurrle ana matumaini kuhusu nafasi ya kikosi chao kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya robo fainali dhidi ya Real Madrid. Wolfsburg wanatarajiwa kwenda katika mchezo huo wa mkondo wa kwanza kesho wakiwa hawapewi nafasi dhidi ya kikosi cha Madrid ambacho kilitoka nyuma na kuichapa Barcelona huku wakiwa pungufu Jumamosi iliyopita. Lakini Schurrle anaamini Wolfsburg ina kila nafasi ya kupata matokeo chanya katika mchezo hui utakaofanyika huko Volkswagen Arena. Akihojiwa nyota huyo wa kimataifa wa Ujerumani amesema sio kweli kwamba hawana nafasi hivyo watu hawapaswi kuwadharau.

No comments:
Post a Comment