Tuesday, April 5, 2016

LUKE SHAW AANZA MAZOEZI.

BEKI wa Manchester United, Luke Shaw ameanza mazoezi kwa mara ya kwanza jana toka alipovunjika mguu miezi saba iliyopita. Beki huyo wa kushoto wa Uingereza mwenye umri wa miaka 20, alivunjika mguu katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya PSV Eindhoven Septemba mwaka jana. Kurejea kwa Shaw kulithibitishwa na mchezaji mwenzake Juan Mata ambaye alituma picha wakiwa pamoja mazoezini katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram. Mata aliongeza maneno katika picha hiyo yakimpongeza Shaw kwa kurejea tena uwanjani baada ya kupita kipindi kirefu.

No comments:

Post a Comment