Monday, April 4, 2016

PIQUE AWATAKA WACHEZAJI WENZAKE KUSAHAU KIPIGO CHA CLASICO.

BEKI wa Barcelona, Gerard Pique amewaonya wachezaji wenzake kuwa mchezo wao war obo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Atletico Madrid utakuwa mgumu zaidi ya ule waliofungw amabao 2-1 na mahasimu wao Real Madrid. Bao la ushindi la Madrid lililofungwa dakika za mwisho na Cristiano Ronaldo lilimaliza utawala wa Barcelona kutofungwa mechi 39, lakini Pique ameendelea kubakia na uhakika kuelekea mchezo wao huo wa kesho katika Uwanja wa camp Nou. Akihojiwa Pique amesema wako vizuri kiali na kimwili na itakuwa muhimu kwao kucheza kwa kiwango bora dhidi ya Atletico baada ya kipigo cha Jumamosi iliyopita dhidi ya Madrid. Beki huyo aliendelea kudai kuwa wanatakiwa waamke kwani mchezo huo hautakuwa rahisi kwani Atletico ni timu ngumu.


No comments:

Post a Comment