HATIMAYE Chelsea imemteua kocha wa timu ya taifa ya Italia, Antono Conte kuwa meneja wao kuanzia msimu ujao. Meneja huyo wa zamani wa Juventus mwenye umri wa miaka 46 anatarajiwa kuanza kibarua chake hicho cha mkataba wa miaka mitatu baada ya michuano ya Euro 2016. Akihojiwa Conte amesema anajivunia kuifundisha nchi yake na sasa ataanza kuinoa Chelsea baada ya michuano ya Ulaya. Guus Hiddink ambaye alichukua nafasi ya Jose Mourinho aliyetimuliwa, anatarajiwa kuendelea kuinoa Chelsea mpaka mwishoni mwa msimu huu. Conte ambaye amenyakuwa mataji matatu ya Serie A katika kipindi cha miaka mitatu aliyoinoa Chelsea, anakuwa meneja wa tano raia wa Italia kuinoa Chelsea baada ya Gianluca Vialli, Claudio Ranieri, Carlo Ancelotti na Roberto di Matteo.

No comments:
Post a Comment