WAKALA wa kiungo wa Manchester City, Yaya Toure jana amesema mteja wake huyo ataondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu kufuatia kutopewa ofa yeyote ya mkataba mpya. Nyota huyo wa kimataifa wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 32, ambaye ni mchezaji bora wa mwaka wa Afrika kwa mara nne mfululizo kuanzia mwaka 2011, alijiunga na City akitokea Barcelona kwa kitita cha paundi 24 Julai mwaka 2010. Miaka sita iliyopita Toure aliuzwa na aliyekuwa meneja wa Barcelona Pep Guardiola ambaye anatarajiwa kuchukua nafasi ya Manuel Pellegrini wakati Mhispani huyo atakapoondoka Bayern Munich mwishoni mwa msimu huu. Wakala wa Toure, Dimitri Seluk amesema wamesubiri kwa kipindi kirefu ahadi ya mkataba mpya kutoka kwa City lakini hakuna chochote kilichofanyika hivyo anadhani mteja wake ataondoka Juni. Toure ameshinda mataji mawili ya Ligi Kuu akiwa na City mwaka 2012 na 2014, Kombe la FA mwaka 2011 na Kombe la Ligi mwaka 2014 na 2016.
No comments:
Post a Comment