MSHAMBULIAJI wa Atletico Madrid, Fernando Torres ameliponda Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA baada ya kutolewa katika mchezo dhidi ya Barcelona, akisisitiza mwamuzi Felix Brych hakuwa tayari kuchezesha mchezo mkubwa kama huo. Torres alitolewa nje baada ya kupewa kadi mbili za njano katika kipindi cha kwanza katika mchezo huo uliofanyika Camp Noun a kuwapa mwanya mabingwa watetezi Barcelona kuibuka kidedea kwa mabao 2-1. Mshambuliaji huyo wa zamani wa Liverpool amekubali kuwajibika kwa kikosi chake kufungwa lakini ameituhumu UEFA kwa kutochagua mwamuzi sahihi kwa mchezo huo. Akihojiwa Torres amesema ni aibu kwa UEFA katika mchezo mkubwa kama huo kushindwa kuweka mwamuzi anayefaa.
No comments:
Post a Comment