Wednesday, April 6, 2016

CESARE MALDINI AAGWA RASMI.

BAADHI ya watu wenye majina makubwa katika soka la Italia jana wametoa salamu zao za heshima kwa nguli wa soka wan chi hiyo na klabu ya AC Milan, Cesare Maldini. Beki huyo wa zamani wa Italia na Milan alifariki dunia Jumapili iliyopita na alikumbukwa na watu wengi waliojitokeza katika mazishi yake jana. Mtoto wa Cesare, Paolo ambaye pia aliwahi kuziwakilisha Italia na Milan kwa mafanikio aliongoza utoaji wa salamu za rambirambi baada ya mazishi kwa kuandika barua ya wazi sambamba na ndugu zake Monica, Donatella, Valentina, Alessandro na Piercesare Maldini. Katika barua hiyo watoto hao walimshukuru baba yao kwa safari ndefu na nzuri waliokuwa naye katika kipindi chote cha uhai wake na kumshukuru kwa kila kitu alichowafanyia katika maisha yao. Wengine waliojitokeza katika mazishi hayo ni pamoja na kiungo wa zamani wa Milan Clarence Seedorf na mkurugenzi mtendaji wa Juventus Giuseppe Marotta ambao nao walitoa salamu kwa nguli huyo.

No comments:

Post a Comment