Wednesday, April 6, 2016

RAMIRES ADAI HIDDINK ALICHANGIA KUONDOKA KWAKE.

KIUNGO wa zamani wa Chelsea, Ramires amedai alilazimika kuondoka Chelsea kutokana na meneja wa muda Guus Hiddink kukataa kumpa muda wa kucheza. Nyota huyo wa kimataifa wa Brazil, alikamilisha usajili wa paundi milioni 25 kwenda klabu ya Jiangsu Suning Januari mwaka huu, akiwa mmoja kati ya wachezaji kadhaa kutoka nchi za Amerika Kusini walioamua kwenda kucheza soka China. Akihojiwa kuhusiana na suala hilo, Ramires ambaye alikaa Chelsea kwa kipindi cha miaka sita, amesema ni mambo binafsi kati yake na Hiddink ndio yaliyochangia yeye kuondoka. Ramires amesema toka Hiddink alipochukua nafasi ya Jose Mourinho, alikuwa akikosa muda wa kucheza jambo ambalo lilimfanya kufikiria kwenda mahali pengine.

No comments:

Post a Comment