NYARAKA zilizovuja zimebainisha kuwa rais mpya wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Gianni Infantino alisaini mkataba na wafanyabishara wawili ambao wamekuwa wakihusishwa na tuhuma za ufisadi. Wafanyabiashara hao, Hugo na Mariano Jinks walinunua haki za kurusha matangazo ya soka ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na kuuza haki hizo baadae kwa bei mara tatu ya ile waliyonunulia awali. Mkataba huo ulisainiwa mwaka 2006 na Infantino wakati akiwa mkurugenzi wa Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA. Hiyo ni moja kati ya nyaraka milioni 11 zilizovuja kutoka kampuni ya mambo ya kisheria ya Panama ya Mossack Fonseca. Mara ya kwanza UEFA ilikanusha kujihusisha kibiashara na watu 14 waliorodheshwa na FBI katika uchunguzi wake wa kashfa ya ufisadi katika FIFA lakini sasa wamekubali kuuza haki hizo za matangazo kwa mzabuni aliyekuwa juu katika mchakato uliokuwa wa uwazi kwa mujibu wa sheria.
No comments:
Post a Comment